Uwekezaji Mkubwa wa Emirates ni Mapinduzi katika Uhandisi wa Ndege
Kwa hatua ya kimapinduzi iliyojikita katika miundo mbinu ya anga, Shirika la ndege la kimataifa la Emirates limetangaza mipango ya uwekezaji wa dola za Marekani milioni 950. Uwekezaji huu mkubwa una nia ya kujenga kituo cha uhandisi cha hali ya juu katika Dubai World Central (DWC), katika tasnia ya anga.Eneo la mradi huu linaukubwa wa mita za mraba milioni 1, linawakilisha juhudi kubwa katika sekta ya ndege, na kuimarisha sifa ya Dubai kama kitovu cha teknolojia na huduma za anga za kisasa. Kituo hicho Kitaundwa kwa umakini mkubwa kusaidia ndege za Emirates na mahitaji yake ya uendeshaji mpaka miaka ya 2040,ambapo kitakuwa kitovu cha ubora kwa huduma za uhandisi wa anga kibiashara katika Mashariki ya Kati. Pia, kuna uwezekano wa kutoa nafasi kwa mashirika mengine ya ndege, ikiongeza thamani yake kwenye tasnia hiyo. HH Sheikh Ahmed bin Saeed Al Maktoum, Mwenyekiti na Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika la ndege na Kundi la Emirates, alisema, "Uwekezaji mkubwa huu unadhihirisha ima...