FEMALE FUTURE PROGRAMME YAKABIDHI HUNDI YA MILIONI 30 JKCI KUSAIDIA WATOTO WENYE CHANGAMOTO YA MOYO
Na Mwandishi wetu,MwelekeoMedia Dar es salaam Kundi la 11 la Mpango wa Female Future Programme (FFP) limekabidhi hundi ya shilingi milioni 30 kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) kwa ajili ya kusaidia watoto wanaokabiliwa na matatizo ya moyo. Mchango huo umetolewa kama sehemu ya shughuli za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) za darasa la washiriki 162 wa mwaka 2025, ambalo ni darasa kubwa zaidi kuwahi kushiriki katika historia ya mpango huo unaoratibiwa na Association of Tanzania Employers (ATE). Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mtendaji Mkuu wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba-Doran, amesema kuwa Mpango wa Female Future Programme haujikita tu katika utoaji wa mafunzo bali pia unalenga kuwajengea wanawake viongozi uwezo wa kuchukua hatua chanya katika jamii. Alisema hadi sasa jumla ya wanawake 620 wamehitimu kupitia mpango huo. Alifafanua kuwa utekelezaji wa mradi wa CSR ni sehemu ya mafunzo ya kukuza ujuzi wa uongozi wa juu ambayo washiriki wa Kundi la 11 wa...