FCC YATETA NA WADAU WA SEKTA YA MADINI GEITA

Na Mwandishi wetu, MwelekeoMedia 

Ndg. Mgasi Kalindimya,ambae ni mkaguzi wa bidhaa bandia wa Tume ya Ushindani (FCC) amesema wameshiriki katika Maonyesho ya sita ya madini kwa lengo la kutaka kumfikia mtumiaji na mlaji wa bidhaa ambaye anapokea huduma moja kwa moja kutoka Kwa wadhalishaji.

Amesema kuwa wapo kwaajili ya kuangalia watu mbalimbali ambao wanachukua mikopo ya wajasiliamali wadogo wadogo ili kuwasaidia kuwapa elimu ya namna bora ya kutumia mikopo hiyo katika masuala ya teknolojia.


Ameyasema hayo Septemba 24, 2023 AFISA mkaguzi bidhaa bandia wa Tume ya Ushindani (FCC) Mgasi Kalindimya katika viwanja vya maonyesho ya sita ya teknolojia ya madini, yanayoendelea mkoani Geita.

Amesema FCC ni Taasisi ya Serikali ambayo ipo chini ya Wizara ya Viwanda na biashara na inasimamia sheria mbili ambazo watu wanaokuja kwenye maonyesho wanapaswa kutambua hilo.

 "Tunasheria mbili ambazo tunazisimamia sokoni, tunasheria ya alama za bidhaa ambayo hii inatupa nguvu ya kupambana na bidhaa bandia, lakini tunasheria ya ushindani ya mwaka 2003 sheria namba nane ambayo inatupa nguvu sisi ya kusimamia Soko na kuhakikisha kwamba Kunakuwa na ushindani ambao ni wa haki na usawa." amesema Mgasi

Ameongeza kuwa "tunapozungumza ushindani tunamaanisha anayekuja kutembea katika maonyesho haya lazima ajue mshindani ni mtu wa aina gani, mshindani ni watu wawili ambao wanazalisha bidhaa ya aina Moja Kwa mafano Maji, au soda huyu anazalisha bidha ya aina hiyo na mwingine anazalisha bidhaa ya aina Moja huyo ndio mshindani hivyo tunamwangalia mshindani katika jicho la wazalishaji wa bidhaa ya aina Moja.


Ameongeza kuwa Katika maonyesho hayo ya madini Kuna makampuni ambayo yamejikita katika uchimbaji wa madini na hasa kuzalisha bidhaa ya aina moja na wanapopeleka bidhaa hiyo sokono hao ni washindani.

Amesema sheria hiyo ya ushindani ambayo ameitaja inamakatazo ambayo yamewekwa juu yao hivyo kupitia Banda la FCC wananchi wakija watapata elimu na kufundishwa ili kujua sokoni Kuna nini na hupaswi kukaa kikao na mwezako ambao ni mshindani mnafanana kibiashara na kupanga mazao sokoni.

Kuhusu wajasiliamali wadogo hawakatazwi kuungana na kimsingi wananguvu, pia wanapewa kisheria kuweza kuungana ili waweze kukuwa na kuna namna bora ambayo sheria imewekwa hasa katika masuala ya ushindani.

Sheria inapima mitaji yao ambapo sheria inasema kama wamezidi mitaji ya shilingi za kitanzania Bilioni 3.5 wanatakiwa kwenda Tume ya Ushindani ili waweze kupewa baraka na namna bora ya kuweza kuungana lakini Kwa kuwasaidia wajasiriamali wadogo, Tume ya Ushindani inatoa nafasi kwa wale ambao mitaji yao ipo chini ya Bilioni 3.5 waungane na wanaweza kwenda kwao ili kuwashauri.

"Tunawakaribisha sana wakazi wa Geita, kanda ya ziwa kwa ujumla wake kwenye Banda la FCC ili kuweza kujifunza kuhusu sheria hiii ya ushindani lakini faida zinazotokana na sheria hiyo ya ushindani ambapo kuna vifungo vya miaka minne hadi 15 na faini milioni 10 hadi 50 au thamani ya mzigo uliokamatwa unachomwa na kuangalia thamani ya mzigo unaweza kupigwa mara tatu." amesema 

Kwa upande wake Afisa Uhusiano Mkuu FCC Nsajigwa Wilfred amewataka wanageita kutojihusha na bidhaa bandia kwa kuwa wapo hapo tangu tarehe 20 siku ambayo maonyesho yalianza rasmi na waandishi mtakumbuka juzi tumefanya semina kubwa ambayo imehusisha wadau mbalimbali kwa lengo la kutoa Elimu mbalimbali kuhusu Tume ya Ushindani kwa wadau wa Sekta ya Madini katika Maonyesho ya sita ya Madini.



Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE