KAMPUNI YA FEMA YAJIPAMBANUA KIVINGINE MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA

Na Prosper Rutayuga, MwelekeoMedia





KAMPUNI ya FEMA Mining and Drilling  LTD inayojihusisha uchimbaji,uchongaji na ulipuaji wa madini nchini iliyopo Munekeze-Katoro Mkoani Geita wameishukuru serikali ya awamu ya sita(6) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Hassan Suluhu kwa kuwapa fursa na nafasi kampuni za kizawa kufanya kazi katika migodi iliyopo nchini.

Akizungumza katika maonesho ya sita yakimataifa ya teknolojia ya madini  yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita Mratibu mradi kutoka Kampuni FEMA MINING AND DRILLING LTD  Mhandisi Jacquline Mtei amesema kuwa kwa sasa milango yakufanya kazi wazawa na kupewa kazi mbalimbali hasa kwenye sekta ya madini ni dhahiri kuwa sekta hiyo inazidi kukua siku hadi siku.





 " Napenda kumshukuru Rais  Dkt Samia Hassan Suluhu kwa kuweza kutengeneza Mazingira ya uwezekano wa wazawa 'makampuni mama' kuweza kufanya kazi katika migodi yetu hii ya kati pamoja na Migodi  mikubwa,Kupitia kampuni  yetu ya FEMA sisi ni kampuni zawa kampuni ya kitanzania  kwa hiyo tumeona mama alivyotengeneza mazingira ambayo imetuwezesha kapata zabuni katika migodi ya kati na mikubwa" Amesema Jacquline

Amesema Sekta ya madini inaoongoza kwakuchangia uchumi wa nchi hivyo inapotokea milango inapofunguliwa kwa wazawa kufanya kazi katika migodi hii pia itasaidia kukua zaidi kwani watatanguliza uzalendo katika nchi yao.

Aidha amewaaalika wanawake kusoma masomo ya sayansi hasa kuhusu miamba na madini kuwa wasiogope kazi zipo pia waondoe dhana potofu kuwa kazi zinazohusu madini ni wanaume pekee.



"fursa za  ajira kwa  wanawake katika sekta ya madini zipo sisi  kampuni yetu imeweza kutusaidia sisi wanawake kupata  ajira zaidi ya wanawake kumi na tano wamepata ajira nikiwemo mimi kwa hiyo wanawake wenzangu msiogope tuje huku"amewahasisha Jacquline


Kwa upande wake Afisa manunuzi na usambazaji kutoka FEMA Mining and  Drilling  LTD Frank Joseph amesema hao kama FEMA wameweza kushirikiana na makampuni tano tofauti  katika kuwapa  zabuni katika kampuni yao kama vile usambazaji wa vipuri,mafuta na virainisha kwa ajili ya mashine zao  pia pamoja na  huduma zingine ikiwemo  usafi,chakula na huduma nyingine za kijamii.

Aidha ameongeza pia katika katika kurudisha shukrani kwa jamiii kwa kile wanachokipata pia wameweza kusaidia kununua madawa katika zahati zinazo zunguka mgodi sanjari na kujenga shule na kukarabati vyumba vya madarasa ikiwemo kuzalisha ajira kwa vijana zaidi ya miamoja wanaozunguka mgodi.

Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE