MAVUNDE AIPONGEZA KAMPUNI YA BLUE COAST KWA UTENDAJI WAKE ULIOTUKUKA


Na Prosper Rutayuga,MwelekeoMedia 

Serikali imesema itaendelea kusimamia sheria ya Local contect ili kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali zao ikiwemo madini ya dhahabu .

Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini  Antony Mavunde alipomtembelea mmoja wa wawekezaji wazawa mkoani Geita ,Athanas Inyasi  anaemiliki kampuni ya blue coast  ili kujionea namna alivyonufaika  na sheria ya Local contect ambapo amewasisitiza wafanyabiashara ,wachimbaji kujitokeza kuomba zabuni .


"Nitoe rai kwa makampuni mengine yakitanzania kuchangamkia fursa hii sisi kama tutahakikisha tunaisimamia sheia hii vizuri ili watanzania wengi  zaidi waweze kunufaika tunahitaji kuwaona  akina mzee Inyasi wengi zaidi kama alivyomsema mkuu wa Mkoa ili mwisho wa siku tuweze kuyaona matokeo ya uchumi wa madini  katika maisha ya watanzania na kupitia uchumi huu tuweze kukuza pia uchumi wa tanzania na jambo hili linawezekana",amesema Mavunde.


Aidha Waziri Mavunde amesema kuwa  uwekezaji wa kampuni ya blue cost umesaidia kutoa ajira nyingi kwa vijana wakitanzania pamoja na kuchangia  mapato ya halmashauri pamoja na  kodi ya Serikali hivyo uwepo wake una maana kubwa katika maendeleo ya nchi na hususani mkoa wa Geita.
 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Makampuni ya Blue Cost ,Athanas Inyasi amesema uwepo wa sheria ya local Contect imesaidia kwa kiasi kikubwa kutokana na kuleta mafanikio makubwa kwa watanzania,huku ajira 360 zikiwa zimetolewa na kampuni hiyo.

"Ninapenda nimshukuru kwa namna ya pekee Rais wa Tanzania mheshimiwa Dkt  Samia Suluhu Hassan anavyoendele kutuwekea mazingira mazuri sisi wafanyabiara na wananchi wote  kwa jumla  na mambo yetu yakaweza kuendelea kukua kitaifa na kimataifa"amesema Inyasi



Awali akitoa taarifa fupi ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Blue Cost  Ndahilo Athanas amesema kampuni yao imejikita pia katika kujenga miundo ya maendeleo kama madarasa na madawati kwa shule za msingi Nyamalembo na Mseto zilizopo mkoani Geita  wakiwa na lengo lakuangalia na sekta nyingine hasa sekta ya afya kwa siku chache za mbeleni.

"Mheshimiwa Waziri kwa kuzidi kutambua umuhimu wa sekra ya elimu  kampuni yetu imetoa mchango wa shilingi milion 150 kupitia mfuko wa GPE Multplier Grant kwa ajili ya uboreshaji wa elimu katika shule za msingi yenye lengo lakutatua changamoto za walimu nchini "amesema Ndahilo

Naye Mkuu wa Mkoa wa geita,Martine Shigela ametumia nafasi hiyo kuwataka wachimbaji wadogo pindi wanapopata fedha waweze kubadilisha biashara ambazo zitawaongezea kipato.



Aidha amesema uwepo wa Local Contect  umeongeza kwa kiasi kikubwa ajira kwa watanzania na kutoa fursa za wazawa kupata manufaa kutokana na shughuli ambazo zinafanyika kwenye maeneo yao.

MWISHO… ili kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali za nchi  ikiwemo madini ya dhahabu .


Mavunde ameyasema haya Septemba 27 ,2023 mara baada ya  kutembelea na kuona uwekezaji mkubwa wa wazawa uliofanywa  mkoani Geita  na  Athanas Inyasi  anayemiliki kampuni ya blue coast.

" Nitoe rai kwa makampuni mengine ya kitanzania kuchangamkia fursa hii sisi kama Serikali  tutahakikisha tunaisimamia sheria hii vizuri ili watanzania wengi  zaidi waweze kunufaika"Amesema 

Nakuongeza " tunahitaji kuwaona  akina mzee Inyasi wengi zaidi kama alivyosema mkuu wa Mkoa Martine Shegela  ili mwisho wa siku tuweze kuyaona matokeo ya uchumi wa madini  katika maisha ya watanzania na kupitia uchumi huu tuweze kukuza pia uchumi wa tanzania na jambo hili linawezekana",amesisitiza  Mavunde.

Pia  Waziri Mavunde ameongeza  kuwa  uwekezaji wa kampuni ya blue cost umesaidia kutoa ajira nyingi kwa vijana wakitanzania pamoja na kuchangia  mapato ya halmashauri pamoja na  kodi ya Serikali hivyo uwepo wake una maana kubwa katika maendeleo ya nchi na hususani mkoa wa Geita.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Makampuni ya Blue Cost ,Athanas Inyasi amesema uwepo wa sheria ya local Contect imesaidia kwa kiasi kikubwa kutokana na kuleta mafanikio makubwa kwa watanzania,huku ajira 360 zikiwa zimetolewa na kampuni hiyo.

"Ninapenda nimshukuru kwa namna ya pekee Rais wa Tanzania mheshimiwa Dkt  Samia Suluhu Hassan anavyoendele kutuwekea mazingira mazuri sisi wafanyabiara na wananchi wote  kwa jumla  na mambo yetu yakaweza kuendelea kukua kitaifa na kimataifa"amesema Inyasi

Awali akitoa taarifa fupi ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Blue Cost  Ndahilo Athanas amesema kampuni yao imejikita pia katika kujenga miundo ya maendeleo kama madarasa na madawati kwa shule za msingi Nyamalembo na Mseto zilizopo mkoani Geita  wakiwa na lengo lakuangalia na sekta nyingine hasa sekta ya afya kwa siku chache za mbeleni.

" Ndugu Waziri kwa kuzidi kutambua umuhimu wa sekra ya elimu  kampuni yetu imetoa mchango wa shilingi milion 150 kupitia mfuko wa GPE Multplier Grant kwa ajili ya uboreshaji wa elimu katika shule za msingi yenye lengo lakutatua changamoto za walimu nchini "amesema Ndahilo

Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita,Martine Shigela ametumia nafasi hiyo kuwataka wachimbaji wadogo pindi wanapopata fedha waweze kubadilisha biashara ambazo zitawaongezea kipato.

Pia amesema uwepo wa Local Contect  umeongeza kwa kiasi kikubwa ajira kwa watanzania na kutoa fursa za wazawa kupata manufaa kutokana na shughuli ambazo zinafanyika kwenye maeneo yao.


Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE