MBUNGE KANYASU AWAPONGEZA WAANDAAJI WA MAONESHO YA 6 YA TEKNOLOJIA YA MADINI

Na Mwandishi Wetu,MwelekeoMedia 

Mh. Constantine John Kanyasu,Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini amewapongeza waandaaji wa Maonyesho ya 6 ya kimataifa ya Teknolojia ya madini na pia kupata nafasi ya kuwa Mgeni mahususi katika kutembelea mabanda mbalimbali yaliyoko katika Maonyesho hayo

Ambapo amesema Maonyesho yameandaliwa vizuri na washiriki ni wengi hivo inatia hamasa, hususani ushiriki wa bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi umeongezeka,  pia kuongezewa Kwa makampuni ya Madini hasa wanaonyesha Teknolojia ya Madini.


Kanyasu amesema Kwa mara ya kwanza Maonyesho hayo yameleta Watanzania wanaochimba Madini kutoka Mikoa nanhata nje ya nchi  kuja kutangaza Biashara zao Tanzania, hivyo amewapongeza waandaaji Kwa jambo hilo kubwa na muhimu.

" Lakini pia kwa mara ya kwanza Maonyesho hayo yameleta Watanzania wanaochimba Madini kutoka Mikoa mbalimbali  na hata nje ya nchi kuja Tanzania kutangaza biashara zao, hivyo niwapongeze sana wandaaji Kwa jambo hili kumbwa na muhimu" amesema Mbunge Kanyasu.



Aidha amesema jambo pekee ambalo wananchi wanatakiwa kujua ni kwamba bado walengwa ( wachimbaji wenyewe ) ado hawajafikiwa  kiasi cha kutosha.

" Ziko Kampuni ambazo lazima wawafuate wachimbaji madogo kule chini, Maonyesho haya hawawalengi makampuni makubwa kama GGM, Bakrifu, na Sota Mining, yanalenga wachimbaji wadogo kwahiyo tuangalie namna ya kuwafuata wale wachimbaji wadogo kule chini hasa  kwenye kuwapeleka Teknolojia, mitaji, lakini kwenye kuwawekea bima" amesema Kanyasu.

" Keasababu mabosi wamekuja hapa,  lakini wale wachimbaji wenyewe wako kwenye mashimo, ambao hata hawajapata nafasi ya kuja  kuona Maonyesho haya, na ndio wanaokufa Kwa kuangukiwa na miamba" ameongeza Mbunge  Kanyasu

Aidha amesema kadiri inavyoonekana  Geita ilivyo sasa sivyo ilivyokua zamani, kuanzia Kasama mpaka Geita amjini palikua na msitu Mkubwa sana, lakini  miti yote imekwisha kwasababu ya Uchimbaji wa madini ( Matumizi ya Matimba) ambapo amesema iko haja ya kutafuta Teknolojia itakayookoa Misitu itakayobaki ili tusiendelee kukata miti yote inayobaki tutaharibu hali ya hewa.



"Kuna uhusiano mkubwa wa hali ya hewa ya Kanda ya ziwa na Misitu ya asili iliyokuwepo, kwahiyo tuchimbe Madini tutengeneze pesa, zile pesa zirudi kupanda miti, kazi nzuri imefanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii pale mbele ya Katolo ule msitu wa Bihalamulo wamepanda hekta 69,000 pale wamepanda msitu mkubwa, ifanyike hivyo kwenye maeneo yote yaliyokua na msitu wa asili lakini imevunwa kwenda kwenye madini kwaajili ya kufidia ile Misitu ambayo imeharibika, mimi nafikiri kwakufanya hivyo tutaendelea kuwa salama zaidi kwa hali hiyo" amefafanua Kanyasu.

Ameiomba Wizara ya madini kuhakikisha kwenye Maonyesho kama hayo mwakani, tuwe na Banda linaloonyesha bidhaa mbalimbali zilizokamili za mawe aina mbalimbali, maana tulipofanya Maonyesho ya Madini Dar es Salaam tulikua na watengenezaji  wa bidhaa mbalimbali kama mikufu, Mikanda, shanga, heleni, shanga, vitu vingi mbalimbali ambao waliletwa na Wizara.

" Sasa hapa tuna Madini yanayotupwa, kule wanaofanya uchechuaji wanakamata zaidi Dhahabu na Silva, maana Silva nyingí inabaki kwenye tope, waje na Teknolojia ya kukamata silva inayobaki kwenye tope, kwasababu sokoni tunahitaji Silva lakini sio koo kwa mchimbaji, mchimbaji anatafutwa dhahabu kwa hiyo asilimia anayopatikana baada ya kuchenjuliwa ni ile ambayo imekamatwa Kwa bahati mbaya.

Aidha ameiomba Tume ya Madini kuwasaidia kuja na Teknolojia ya kuanza kukamata Silva, dhahabu, yakamatwe na Madini mengine ili tusitupe utajiri huu kwenye matope na Madini mengine kama hapa walivyokuja hapa watu wa Tanzanite kutoka Mirerani tumefurahi sana, kwasaba na Geita yapo mawe aina hii ambayo yanaweza kufanyika nakshi watu wakanunua wakavaa, wakaacha kuvaa  maplastiki.

Naye mfanyakazi wa Kampuni ya uchimbaji Madini ya Tanzanite ya Franone Mining & Gems Company Ltd Furaha  Mshai amesema ujio wao kwenye Maonyesho hayo ni fulsa pekee ya kutangaza Madini yao aina ya Tanzanite na kuwaonyesha Watanzania Madini  pekee yanayopatikana  hapa nchini ambayo ni  Tanzania.




Mshai amesema  Madini hayo yamekua ni kivutio kikubwa katika Maonyesho hayo yamekua ni utajiri mkubwa wa nchi ya Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE