NSSF YAJIVUNIA KUONGEZA THAMANI YA MFUKO

Prosper Rutayuga, MwelekeoMedia 

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)  Masha Mshomba amesema ,katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  imeweza kuongeza thamani ya Mfuko huo kutoka Trilioni 4.8 Hadi kufikia shilingi Trilioni 7.6 kwa hesabu zinazoendelea kukaguliwa Hadi hivi sasa.

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo mbele ya  Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt.Dotyo Biteko  alipotembelea Banda hilo ambapo aliipongeza NSSF kwa hatua hiyo.




Masha amesema kuongeza thamani ya Mfuko Hadi kufikia kiasi Cha shilingi Trilioni 7.6 ni hatua kubwa .

"Thamani ya Mfuko imeendelea kukua  kwa kasi tukizungumzia mahesabu yaliyokaguliwa  hadi mwaka jana Juni,tuliuwa na mahesabu ya shilingi trilioni 6.08,lakini kwa mwaka  huu mpaka kufikia mwezi Juni mwaka huu hesabu ambazo bado zinaendeea kukaguliwa thamani ya Mfuko ni shiingi triioni  7.6"amesema na kuongeza kuwa
“Ni ukuaji mkubwa sana hasa ukizingatia kwamba kabla Rais Samia hajaingia madarakani thamani ya mfuko ilikuwa ni shiingi triioni 4.8 tu."




Akizungumza kuhusu uwepo wao katika maonesho ya Madini amesema wapo kwa sababu ya kuelimisha wadau na wananchi kwa ujumla ilinwaweze kujiunga na Mfuko huo Ili kuendelea kuongeza wananchi na thamani ya Mfuko.

"Katika maonesho hayo tumekuwa na mafanikio makubwa ,tumeongeza wachangiaji wa NSSF ambapo kwa mkoa wa Geita tunakusanya shilingi bilioni  96 ,lakini wakati   Rais Samia anaingia madarakani kwa mkoa huu tulikuwa tunapokea michango ya shilingi  bilioni  26 tu,tunaamini tutaendelea kufanya vizuri zaidi katika miaka ijayo."



Aidha amesema Mfuko kwa ujumla tumeuwa pia na 'perfomance' nzuri sana ambapo mwaka  unaoishia Juni  2023  thamani ya  michango ilikuwa shilingi Trilioni  1.66 na shilingi Trilioni 1.48  kwa mwaka ulioishia Juni 2022 .

Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE