RITA - WANANCHI KUWENI NA DESTURI YA KUANDIKA WOSIA ILI KUONDOA MIGOGORO
Na Mwandishi wetu, Mwelekeomedia
WAKALA Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) umewataka wananchi Kujenga desturi ya kuandika wosia Ili kuondoa migogoro ya mirathi inayochukua muda mwingi kufuatilia kes mahakamani badala ya muda huo kuutumia kwenye shughuli za uzalishaji Mali.
Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali kutoka RITA Rwegasira wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye maonesho ya sita ya Kimataifa na Teknolojia 2023 mkoani Geita.
"Sisi tuna kaulimbi inasema 'kuandika wosia siyo uchuro'ikiwa na maana kwamba kuandika wosia ni utaratibu ambao binadamu anatakiwa awe nao ili kujua siku asipokiwepo mali zake zinagawanywa katika utaratibu bila kuleta migogoro."amesema Rwegasira na kuongeza kuwa
"Tunashuhudia katika vyombo vya habari watu wanagombania Mali alizoacha marejemu lakini kumbe angekuwa ameacha waraka kwamba Mali zinagawanywaje migogoro kwenye jamii isingekuwepo na watu wasingetumia muda miwngi kugombana kwa kwenda mahakamani kudai mali ambazo zingegawanywa kwa utaratibu unaoeleweka"
Aidha amesema pamoja na kutoa huduma nanushairi katika kuandika wosia pia RITA inajihusisha na usajili wa matukio mbalimbali ya binadamu ikiwemo kuzaliwa,kufa ,ndoa na talaka , huduma za kuasili watoto.
Vile vile amesema RITA inatoa huduma ya ushauri katika suala la ufilisi na masuala ya bodi za wadhamini.
"Kwa hiyo kwa kifupi sisi kama RITA tunahudumia watu wengi ambao wanakuja hapa wanahitaji kusajili vyeti vya kuzaliwa ambavyo vinasaidia katika mchakato mzima wa kupata huduma nyingine kama kitambulisho Cha utaifa ( NIDA) , namba za utambulisho wa mlipa Kodi na masuala mengine ambayo yanasaidia kupata hati za kusafiria,
"Kwa hiyo ukiangalia kwa upana wake hizo huduma zinawahusu pia wachimbaji na wafanyabiashara kwa sababu wakiwa wamesajiliwa maana yake wametambuliwa, basi Serikali inapata nafasi ya kuwatambua watu inayowahudumia katika sekta mbalimbali zikiwemp sekta za madini."
Ameongeza kuwa "Niseme tu RITA imehamia Geita vyeti vya kuzaliwa vinatolewa kama mnavyoona ndani ya muda mfupi kikubwa aweze kufika na viambatanisho stahiki vinavyowezesha kupata huduma ya cheti Cha kuzaliwa ."
Naye mwananchi aliyekuwa katika Banda hilo akipata huduma Lilian Ndila ameishukuru Serikali kwa kuleta maonesho hayo kwani yanasaidia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata vyeti vya kuzaliwa kwa urahisi.
"Mimi nashukuru Leo nimepata cheti cha kuzaliwa cha mwanangu kwa siku mbili tu ,wakati nimeshafuatilia kwa takribani miezi miwili bila mafanikio."amesema Ndila





Comments
Post a Comment