SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUENDELEZA MILKI NCHINI
Na Mwandishi Wetu, MwelekeoMedia
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia vifungu vyake imeona haja ya kushirikiana na Sekta binafsi ili kuendeleza miliki nchini.
Hayo yamebainishwa Jana na Kaimu Meneja Mawasiliano na Masoko Wakala wa Majengo Tanzania (TBA ) Fredrick Kalinga mbele ya Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu alipokua akitembelea mabanda ya Maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini chini ya kauli mbiu " Matumizi ya Teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira" yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili Halmashauri ya Mji Geita.
Kalinga amesema Serikali ya awamu ya sita kwa kuona haja ya kuhuisha Sheria iliyoanzisha Wakala wa Majengo Tanzania ( TBA ) kwa kuiboresha kupitia GN namba 595 Agosti 25, 2023 ambayo inairuhusu TBA kushirikiana na Sekta Binafsi kuendeleza miliki nchini (kujenga nyumba za kupangisha na kuuza kwa wananchi wote)
" Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuona haja ya kuhuisha Sheria iliyoanzisha Wakala wa Majengo Tanzania ( TBA ) kwa kuiboresha kupitia GN namba 595 a tarehe 25 Agosti 2023, ambayo inairuhusu TBA kushirikiana na Sekta Binafsi kuendeleza miliki nchini (kujenga nyumba za kupangisha na kuuza kwa wananchi wote) " amesema Kalinga.
Aidha Kalinga amesema Kwakufanya hivyo itakua nafasi nzuri ya kuendeleza majengo mengi zaidi na wanatarajia taasisi itaongezeka, hivyo Sekta binafsi muda si mrefu wataarifiwa namna gani watashirikiana na Wakala wa Majengo Tanzania ( TBA )
Akijibu hoja ya Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu aliyetaka kujua ni lini TBA itaanza kujenga Majengo mbalimbali katika Jimbo la Geita Mjini, Kalinga amefafanua kwenye bajeti ya Mwaka huu wanatarajia kuanza kujenga jengo Moja la gorofa karibu na " raund about" eneo maarifu msikitini.
" Pale tunategemea tutajenga jengo la gorofa moja ambalo chini litakuwa eneo la Biashara, na juu litakuja eneo la Makazi, huo ndio Mpango wa TBA katika Jimbo la Geita Mjini.
Akizungumzia uwepo wa TBA kwenye Maonyesho hayo amesema pamoja na hayo wamekwenda kuwaonyesha wananchi wa Mkoa wa Geita miradi ambayo Taasisi yao inatekeleza hasa maeneo haya ya Chato.
Aidha amesema ipo miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na mingine tayari imekamilika kama hospitali ya rufaa ya Kanda ya Chato, hospitali ya rufaa ya Mkoa, majengo ya Ofisi ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa.
"Vile vile tunawaonyesha wananchi kwamba Serikali imehamia Dodoma na serikali imewekeza fedha nyingi kwenye Ujenzi wa Mji wa Serikali, hivyo tumekua tukiwaonyesha majengo ambayo yanajengwa katika Mji wa Serikali" amesema Kalinga.
"Karibuni sana Geita, na nawapongeza kwasababu nawaona kila Mwaka, kwa bahati nzuri mko Geita na kazi yenu nzuri, nimefika Chato, nimefika hospitali ya Mkoa, Mwaka jana nilipowatembelea nilitamani kujua nje ya miradi ya pengine hamfikirii kufanya hivi kwenye Mikoa kama Geita? alihoji Mbunge Kanyasu.




Comments
Post a Comment