BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO YAWAHAKIKISHIA SOKO LA UHAKIKA WAKULIMA NCHINI

Na Mwandishi Wetu, MwelekeoMedia 

Francisco Amos,Afisa mauzo na usambazaji kutoka Bodi ya nafaka na  mazao mchanganyiko Kanda ya ziwa amesema licha ya kuwa ni mara Yao ya kwanza kushiriki maonesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini mkoani Geita,wameridhishwa na ubora wa maonesho hayo kwani yamewakutanisha na wadau wapya ikiwa ni pamoja na kujipanua zaidi kwa wananchi.

Amesema kuwa wananchi wengi walipata fursa ya kufika kwenye Banda lao na Kwa ujumla walipenda huduma na bidhaa ambazo walikuja nazo kwenye maonyesho hayo.


Amos ameyasema hayo septemba 30 mwaka huu katika hitimisho la maonyesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini ambayo yanafanyika Kila mwaka mkoani humo .

Amos Amesema licha ya kwamba ni mara yao ya kwanza kushiriki kwenye maonyesho hayo lakini yamewapa picha nzuri kwamba wakati mwingine waje vizuri zaidi  nakwamba  wananchi wamependa bidhaa na huduma na wameonyesha uhitaji mkubwa zaidi.


"Kwakifupi naweza kusema maonyesho yamekuwa tofauti na tulivyotarajia kwani tulikuja kama kuona kama bidhaa watazipenda lakini kimsingi majibu yamekuwa mazuri na wametembelea wengi na bidhaa zimechukuliwa za kutosha na tumepata mawakala wa kutosha na wasambazaji wengine wakutosha."Amesema Amos 

Amesema kuwa meseji kubwa ambayo inapelekwa Kwa wanageita na Kanda ya ziwa ni kwamba hasa wakulima na wadau wote ambao wanahusika katika sekta ya nafaka na kilimo Kwa ujumla ni  Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko imetengenezwa maalumu au kuundwa maalumu Kwaajili ya kuja kuwa Jukwaa litakalokuja kuwanufaisha  wakulima .


Ameongeza kuwa anatoa wito Kwa wakulima waendelee kulima mazao yao kisasa waendelee kuboresha mashamba yao na vitu mbalimbali vinavyotimika kwenye kilimo ili waendelee kupata mazao ya kutosha kwani Soko la bidhaa zao lipo na Bodi ya nafaka ni Jukwaa muhimu sana na lina maana sana ambapo wao wanaweza kuuza mazao yao hivyo wanageita na watanzania waendelee kulima na baada ya hapo bidhaa zao zipo kwenye supermarket na maduka mengine zitapatikana na Kwa Bei nafuu kabisa .

"Uhakika wa bidhaa upo na wakati mwingine tutakuja vizuri zaidi na bidhaa nyingi ambazo wananchi wameziulizia  na kuhusu changamoto wananchi wengi wanakosa elimu ya kutosha hasa inapofika suala la ubora wa chakula na wanamitazano furani kuhusu ubora wa chakula hivyo  wakati mwingine tutakuja vizuri zaidi na kuwaeleza wananchi kuhusu ubora wa chakula lakini pia kuwajengea uwezo wa uelewa zaidi 



Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE