MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NCHINI AMEITAKA KAMPUNI YA SUMAJKT BOTTLING LTD KUONGEZA UBINIFU NA UBORA WA BIDHAA .

 Kampuni ya SUMAJKT Bottling co. Ltd, inayozalisha maji ya Uhuru Peak Pure Drinking Water, imezindua mikondo miwili ya uzalishaji maji na Muonekano mpya wa chupa za maji ya Uhuru Peak, 

Akizungumza jijini Dar es Salaam Leo Octoba 16 Mkuu wa wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali CDF Jacob John Mkunda amesema  Serikali ina matarajio makubwa na Jeshi la kujenga Taifa JKT na Jeshi la wananchi.

Amesema  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatambua na kutembea kifua mbele kutokana na mchango mkubwa unaotokana na shughuli zinazofanywa na  Jeshi hilo hasa katika swala zima la malezi kwa vijana.


Jenerali Mkunda amefafanua kuwa  kutokana na Serikali kutambua Mchango wa Jeshi hilo imeweza kulipatia Jeshi hilo la  Suma Jkt mradi wa ujenzi wa nyumba 5000 Jijini  Dodoma na Mradi wa kulinda bomba la Mafuta hoima.

Jenerali Mkunda ametoa wito kwa Suma Jkt kuendelea kubuni mikakati zaidi na kuboresha bidhaa ili  ziweze kukidhi soko la ndani na nje ya nchi kwa kuzingatia ubora wa maji ili wateja wafurahie na kuongeza mapato.

Pia amewataka kuendelea kufanya kazi kwa weledi na bidii na kuitunza Miundo mbinu ikiwemo  kufanya biashara hiyo kwa faida na sio kwa hasara.

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa  JKT Kanali Petro Ngata  amesema kuwa uwepo wa Mikondo hiyo ya uzalishaji maji utaongeza wigo katika Sekta ya maji biashara na ongezeko la wateja katika biashara ambapo utaongeza mapato.


Amesema mkondo wa kwanza unazalisha maji ya 350ml,600,1.6lita,1lita na una uwezo wa kuzalisha lita 10,000 kwa saa ambapo mkondo wa pili una uwezo wa kuzalisha chupa za maji 500 kwa saa na unazalisha maji lita 13,na lita 18. 

Naye Mkuu wa tawi la utawala Jkt Brigadier Jenerali Hassan Mabena  akimwakilisha Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele  amesema kiwanda hicho kilianza uzalishaji Mwaka 2018 na kwa kuona kuwa uzalishaji wake ni mdogo ndipo wakaamua kufanya maboresho ili kukiongezea uwezo katika uzalishaji kwa kuongeza mitambo miwili ya uzalishaji yenye uzalishaji unaoanzia Mils 360,600,lita 1,lita1.6,lita 13 na lita 18




Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE