TBA KUSHIRIKISHA SEKTA BINAFSI KWENYE MIRADI


Na Mwandishi wetu,MwelekeoMedia.

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imepanga kushirikisha sekta binafsi katika miradi yao ili kusaidia kuondoa changamoto ya nyumba kwa watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam octoba 16,  baada ya kutembelea miradi mitatu ya TBA,  Mkurugenzi wa Idara ya Miliki  TBA, Said Mndeme amesema kuwa mahitaji ya nyumba yamekuwa yakiongezeka kila mwaka.

"Machi mwaka jana Rais Dk.Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa nyumba za Magomeni Kota, alitutaka TBA na taasisi nyingine za Serikali zinazioshughulikia ujenzi wa makazi ya watu kushirikiana na sekta binafsi za nje au ndani kwani  Kwa kufanya hivyo zitaweza kuendeleza makazi bora kwa haraka kuliko kusubiri Serikali kukusanya fedha ambazo haziwezi kukidhi uhitaji wa haraka wa makazi hayo, " amesema.


Amesema agizo hilo la Rais Dk. Samia liliungwa mkono na wabunge  ambao  waliishauri TBA, kushirikiana na sekta binafsi ili kuongeza uwezo wa kujenga nyumba nyingi zitakazosaidia kupunguza uhaba kwa watumishi wa umma badala ya kuendelea kutegemea ruzuku ya serikali.

Ameongeza kuwa machi mwaka huu Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliishauri TBA kuanza kujiendesha kibiashara kwa kushirikiana na Sekta Binafsi na kuacha kutegemea fedha za ruzuku kutoka Serikalini kutekeleza miradi yake.

Mndeme amesema kwa miaka iliyopita mahitaji ya nyumba yalikuwa yakiongezeka taratibu ila kwa sasa uhitaji ni mkubwa.

"Kwa sasa tunakamilisha miradi hii taratibu  kwa kuwa Serikali imepitisha mabadiliko ya kuturuhusu kushirikiana na sekta binafsi, tutatoa  orodha ya miradi yote Tanzania  nzima na tutawakaribisha sekta binafsi  ili kuweza kuja kushirikiana na sisi katika uendelezaji wake,”amesema.

Amesema yapo maeneo mengi ambayo hivi karibuni watayatangaza na kuzikaribisha sekta binafsi kushiriki katika kuyaendeleza.

 "Eneo la Canadian village tunatarajia kujenga majengo 23 yatakayobeba familia 472  na nyumba hizi zitatumiwa na wananchi wote, hivyo tunazikaribisha sekta binafsi kushirikiana   kuendeleza eneo hilo," amesema .

Pia ameongeza kuwa kabla ya mwaka huu kuisha wanatarajia kutangaza miradi mipya  katika eneo hilo la Canadian lililopo Masaki, Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja TBA Mkoa wa Dar es Salaam, Benard Mayemba amesema utekelezaji wa miradi ya  Dar es Salaam inakwemda vizuri hivyo nimatumaini yao miradi itakapokamilika itatatua changamoto ya nyumba za makazi kwa watumishi wa umma na wananachi wote kwa ujumla.

" huu ujenzi wa nyumba awamu ya pili zilizopo magomeni Kota utekelezaji wake ni asilimia 83 na nyumba hizo zitakaliwa na wananchi wa kipato cha kati kuelekea juu ," amesema.

TBA inaishukuru serikali kwa kutoa  sh.bilioni 69.2 Kwa ajili ya miradi ya maendeleo pekee ikiwa pamoja na ukarabati wa majengo.kutokana na uwepo wa ongezeko hilo,mahitaji ya nyumba yamekuwa makubwa, hivyo wanaangalia  maeneo ya kuzishirikisha sekta binafsi katika kuendeleza miradi yao .

Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE