NDUGU ABASI MTEMVU ACHANGISHA HARAAMBEE MAALUM KATIKA KANISA LA WAADVENTISTA
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Abas Zuberi Mtemvu na MNEC wa CCM Mkoa Juma Simba Gadafi Pamoja na Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Kinondoni Shaweji Mkumbura wamehudhuria Ibada ya Kanisa la Adentista wa Sabato Yombo Dovya Wilaya ya Temeke. Katika ibada hiyo M/kiti wa Ccm Mkoa Abas Zuberi Mtemvu Amealikwa ili Kanisa hapo kwa Lengo la Kufanya Haraambee Maalum ya Kuchangia Ujenzi wa Kanisa hilo Pamoja na Vifaa vya Kisasa Kwaajili ya Kwaya Katika hapo. Kupitia haraambee hiyo Mwenyekiti aliifanikiwa Kuchangisha fedha taslim Shilingi Milioni 11,000,000 na ahadi Shilingi 9,000,000 Viongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabado Dovya Wamemshukuru Abas Mtemvu kwa Kuwa na Moyo wa Kujitolea Pamoja na Kukubali Mualiko wa Kuwa Mgeni Rasmi Katika haraambee hiyo.