SIKU YA MISITU NA UPANDAJI MITI KITAIFA KUFANYIKA WILAYANI SAME



  Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline 
        
MAKAMU wa Rais Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Misitu na Upandaji miti duniani ambayo kitaifa itafanyika Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Same machi 21 mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu akiwa Wilayani Same kwenye ziara ya kukagua eneo litakalofanyika maadhimisho hayo pamoja na kukagua miradi ya maendeleo atakayotembelea Dkt. Mpango

Babu amewataka wakazi wa Same na maeneo ya jirani kutumia vizuri nafasi ya kuwepo tukio hilo kubwa la kitaifa la maadhimisho ya siku ya Misitu na Upandaji Miti kushiriki kikamilifu ikiwemo kupanda miti kama sehemu ya kuunga mkono kampeni za kitaifa za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni ameziomba kamati za maandalizi kufika kwa wakati eneo la tukio ili kushirikiana kwa pamoja na watendaji wengine wa Wilaya na Halmashauri sskuhakikisha maandalizi yanakamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa.

Maadhimisho hayo yataanza rasmi Machi 18 kwa kufanya shughuli mbali mbali ndani ya Wilaya ikiwemo utoaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi pamoja na miti inayopaswa kupanda kwenye maeneo yao kulingana na mazingira yake.






Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE