Posts

Showing posts from April, 2024

HUU HAPA UJUMBE WA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, MUUNGANO DAY

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline  “Nawatakia Watanzania wote kheri ya kutimiza miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, kwa niaba yenu Watanzania nawashukuru kwa dhati Waasisi wa Muungano Mwl.Nyerere na Mzee Karume pamoja na Viongozi waliofuata baada yao kwa kutuleta pamoja na kujenga Taifa huru, madhubuti na lenye matumaini , zawadi pekee tunayoweza kuwapa ni kuendelea kudumisha Muungano huu na kuyaenzi maono yao kwa msemo wa siku hizi tunasema tuwape maua yao” “Waswahili tunaamini shughuli na kama mnavyoona pamoja na baraka ya mvua lakini Watu wamejitokeza kwa wingi kwenye shughuli hii, tumepata heshima ya kuungwa mkono na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka SADC na Jumuiya ya Afrik Mashariki na wapo Viongozi waliokuja kuwawakilisha Marais wa Nchi zao" - Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

TAKUKURU YAONYA WATAKAOHUJUMU MIRADI YA RAIS SAMIA

Image
Na Allan Vicent,DmNewsOnline TABORA  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Tabora imetoa onyo kwa wale wote watakaobainika kufuja mali za umma au kutumia vibaya fedha za miradi ya maendeleo zinazotolewa na serikali ya awamu ya 6. Onyo hilo limetolewa na Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoani hapa Mhandisi Abnery Mganga alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana ambapo alibainisha kuwa wamejipanga kufanya ufuatiliaji wa kina wa miradi yote. Ameeleza kuwa katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni 2024 wamejipanga kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kudhibiti vitendo vya rushwa kwa kufanya ufuatiliaji wa kina wa gharama za miradi yote ikiwemo manunuzi yaliyofanywa. Ameongeza kuwa mbali na kufuatilia utekelezaji miradi ya maendeleo katika halmashauri zote 8 za Mkoa huo ili kujiridhisha kama thamani ya fedha imezingatiwa pia watafuatilia mapato ya serikali katika maeneo. ‘Tutachukua hatua stahiki kwa wale wote watakaobainika kufuja mali za umma na kwa kushir...

TFS YAKABIDHI MILIONI 20 KWAAJILI YA KUSAIDIA WANANCHI WA RUFIJI NA KIBITI

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline WAKALA  wa Huduma za Misitu Tanzania - TFS umetoa msaada wa kiasi cha shilingi 20,000,000/= kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko Wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani. Akipokea msaada huo mapema  leo APril  25, 2024 Mkuu wa Mkoa wa Pwani,  Abubakar Kunenge ameshukuru TFS kwa kujali wananchi wakati huu wa changamoto ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea.  "Fedha hizi zitatumika katika kutoa huduma kwa wananchi wanaopitia changamoto ya mafuriko Rufiji na Kibiti na ninaamini hiki mlichofanya kitaenda kutusaidia mbele kuhakikisha mazingira yanatunzwa,” amesema Kunenga Meneja Uhusiano wa TFS Johary Kachwamba akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa uhifadhi Prof. Dos Santos Silayo, amesema TFS inatoa pole kwa waathirika wa mafuriko kwa maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Rufiji na Kibiti, "TFS ina misitu yenye hekta 32,902 ndani ya wilaya ya Rufiji, hivyo wana Rufiji ni Wahifadhi wenzetu na tutaendelea kuwashi...

EMIRATES ANNOUNCES STRATEGIC APPOINTMENTS ACROSS COMMERCIAL OPERATIONS TEAMS

Image
                 MwelekeoMediaOnline  Emirates has announced new movements in its commercial teams across Europe, Africa, and East Asia in line with the airline’s strong growth trajectory.  The new rotations will position emerging UAE National talent in some of Emirates’ key markets, to help the airline achieve its short, medium and long-term goals through navigating various challenges and opportunities.   “We take pride in developing exceptional Emirati talent within our workforce and are committed to supporting their career progression and advancing their leadership capabilities.  Through the new rotation, six prospective leaders will be well-positioned to capitalise on opportunities and overcome industry challenges in their respective markets. I’m confident that our newly appointed managers will not only gain new experiences, but also use their existing knowledge and skills to support our current and future strateg...