HUU HAPA UJUMBE WA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, MUUNGANO DAY
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
“Nawatakia Watanzania wote kheri ya kutimiza miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, kwa niaba yenu Watanzania nawashukuru kwa dhati Waasisi wa Muungano Mwl.Nyerere na Mzee Karume pamoja na Viongozi waliofuata baada yao kwa kutuleta pamoja na kujenga Taifa huru, madhubuti na lenye matumaini , zawadi pekee tunayoweza kuwapa ni kuendelea kudumisha Muungano huu na kuyaenzi maono yao kwa msemo wa siku hizi tunasema tuwape maua yao”
“Waswahili tunaamini shughuli na kama mnavyoona pamoja na baraka ya mvua lakini Watu wamejitokeza kwa wingi kwenye shughuli hii, tumepata heshima ya kuungwa mkono na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka SADC na Jumuiya ya Afrik Mashariki na wapo Viongozi waliokuja kuwawakilisha Marais wa Nchi zao" - Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan



Comments
Post a Comment