SERIKALI YAIPONGEZA ATE KWA MJADALA MUHIMU KUHUSU MATUMIZI YA AKILI MNEMBA,MKUTANO MKUU WA 65 WA MWAKA


Na Mwandishi Wetu,MwelekeoMedia

" Napenda kuwapongeza ATE kwa kuandaa mjadala huu ambao umeweza kutufikirisha katika masuala ya teknolojia.

 Niwaahidi kwamba tuliyojadili nitayawasilisha kwa viongozi wa juu na kuleta ufumbuzi kwenye changamoto.

 Napenda kuasa machache ninapo hitimisha hotuba yangu kwa kusema, tunaposimama kwenye ukingo wa enzi mpya, ni muhimu kukaribisha ujumuishaji wa teknolojia ikiwemo Akili Mnemba (AI) kwa mtazamo wa jumla. 

Utayari wetu mahali pa kazi unazidi maendeleo ya kiteknolojia, unajumuisha elimu, udhibiti, ushirikiano, na ahadi thabiti kwa ustawi wa wafanyakazi wetu.

 Tufikiri katika mapana na kutafuta suluhisho kwa pamoja. Tushirikiane Serikali, Waajiri, Waelimishaji, na wadau wote katika kuhakikisha kuwa Tanzania iko tayari kuendesha safari hii ya mabadiliko.

Nawasihi kila mmoja wenu kuchukua hatua madhubuti katika uwezo wenu kuchangia maono haya.

 Iwe ni kupitia uwekezaji katika teknolojia mpya, kuunda mazingira ya kazi yenye msaada, au kutetea vitendo vya Akili Mnemba vya kimaadili, juhudi zenu ni muhimu. 

Tujenge mustakabali ambapo teknolojia  inaboresha tija na ustawi wetu, huku pia ikilinda afya ya akili na ustawi wa rasilimali" amesema  Patrobas Katambi, Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi,vijana,Ajira na wenye Ulemavu)












Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE