RAIS SAMIA KUWA MGENI RASMI KONGAMANO LA KISWAHILI KUBA



Na Angelina Mganga,DmNewsOnline 
DAR ES SALAAM 

RAIS wa Jamhuri ya Muumgano Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kiswahili litakalofanyika Jijini Havana nchini Kuba kuanzia Novemba 7 hadi 10,2024.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo (BAKITA) Dkt.Damas Ndumbaro  wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 30,2024 Jijini Dar es Salaam. 

Dkt.Ndumbaro amesema kuwa zaidi ya washiriki 600 sawa na asilimia 95 watahudhuria kongamano hilo ambapo zitakuwepo taasisi binafsi,vyuo vikuu na vyama kiswahili kutoka nchi mbalimbali Dunia .

"Tangu mwaka 2021 UNESCO walitambua kiswahili na wakaweka Tarehe 7 kuwa siku ya Kiswahili duniani kwani Chama Cha TANU kiliasisiwa ,kwahiyo lugha ya Kiswahili ni ya Saba dunia watu millioni 500 wanazungumza kiswahili duniani  kwahiyo huu ni muda muafaka wa kukibidhahisha  kiswahili katika mataifa mbalimbali",amesema Dkt. Ndumbaro

Pia amessema washiriki wa kongamano hilo watajigharamia wenyewe kwa Kila kitu.

Aidha amesema Kongamano hilo litafunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel pia kongamano litakuwa na burudani ya vikundi vya Ngoma,semina mbalimbali,uzinduzi wa Kamusi ya Kiswahili kwenda katika Lugha ya Kispaniora kilichoandaliwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam pia litakuwepo onesho la Kanga.

Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE