VETA WASHIRIKI MAONESHO YA TISA YA SAYANSI ,TEKNOLOJIA NA UBUNIFU




Na Angelina Mganga,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM

CHUO cha Ufundi Stadi VETA Dar es Salaam wameshiriki kwenye Kongamano la tisa la Maonesho ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu  linalofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo kwa kipindi cha miaka  mitano wamefanikiwa kuibua bunifu 118 na kati ya hizo 13 zimeingizwa sokoni na 45 zipo katika mchakato wa kuingizwa sokoni.

Meneja Uhusiano kwa Umma Veta, Sitta Peter, ameyasema hayo leo, Desemba 2, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kongamano la hilo.

Meneja Peter amesema kwamba katika bunifu hizo zipo dawa  mbalimbali kama dawa za UTI, fangasi na za kuzuia mbu waenezao malaria .

Pia  amefafanuana kuwaomba  Watanzania kutumia dawa hizo ili kuwaongezea hamasa za kuendelea kubuni dawa nyingine zitakazokidhi mahitaji kwa wananchi.

"Maonesho haya ni moja ya kazi  zetu na sehemu ya kuwaonesha watanzania na jamii kwa ujumla ambavyo tumeweza kufanikiwa katika kufundisha na kubuni bidhaa  mbalimbali ambazo zinaweza kuwa msaada kwa jamii"amesema

  
Mwalimu wa Chuo Cha VETA Dar es Salaam Ally Issa  amesema kutokana na kufanikiwa kubuni bidhaa mbalimbali na tayari wamezipatia hati miliki ili bunifu hizo zisiweze kuchukuliwa au kuigwa na wengine.


Mwalimu Issa ameendelea kwa kusema kwamba  bidhaa ambazo bado hatujaziingiza sokoni tunaendelea na mchakato wa kupata miliki bunifu na tunatumaini kwamba tutafanikiwa.

Kwa upande wake Mvumbuzi wa kifaa cha kufundushia mfumo wa jua na muundo wa Atomu, Ernest Maranya amesema tayari kifaa hicho kimepata ruhusa ya kufundishia kwenye shule za msingi na sekondari baada ya kupata Ithibaki kutoka Wizara ya Elimu.

Mvumbuzi  Maranya ameiomba  Serikali na wadau wa elimu kumsaidia mtaji ili aweze kutengeza kifaa hicho kwa wingi jambo litakalosaidia kufikia malengo ya kutawanywa kwenye shule mbalimbali nchini.

"Kupitia kifaa hiki  ninaamini wanafunzi wengi wataweza kuelewa vizuri somo la mifumo ya jua, hivyo naomba wadau wa elimu wanisaidie mtaji ili niweze kutengeneza kifaa hiki kwa wingi na kiweze kuwafikia wanafunzi wengi na kwa wakati",amesema



Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE