CUF YAMFUTA UANACHAMA MBUNGE WA MTAMBILE VISIWANI PEMBA



Na mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM 

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemfutia uananacha Mbunge wa Jimbo la  Mtambile Visiwani Pemba Seif Salim Seif kwa kile kinachodaiwa amekisaliti Chama hicho na kukiunga mkono Chama tawala cha CCM.


Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa  Chama Cha Wananchi Taifa Profesa Ibrahim Lipumba Januari 12,2025 wakati wa mkutano na wanahabari akitoa taarifa ya maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kilichofanyika Januari 8 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

Amesema Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lilipokea na kujadili video clip yenye maneno ya Hujuma na Usaliti kwa chama,yaliyotolewa na Mbunge wa Mtambile kupitia CUF aliyoyatoa mbele ya vyombo vya habari.

"Mbunge Seif aliwaahidi viongozi wa Chama cha Mapinduzi kwamba atahakikisha CCM inashinda na kuchukua Jimbo la Mtambile kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025 na kwamba kwake CCM ni kama JAHAZI anayolazimika kuipanda ili asiangamie.Maelezo hayo yalitafsiriwa kama Hujuma na Usaliti kwa Chama na kupelekea Mbunge Seif aitwe kwenye kikao Cha Baraza kuu la Chama hicho kuja kujitetea kutokana na  makosa hayo.Baraza lilijadili makosa hayo,mwendelezo wa jumla  wa mbunge huyo na dharau yake kwa Chama na ikiwa ni pamoja na kutoheshimu wito halali wa kuja kujitetea mbele ya Baraza.Baraza limekubaliana kwa kauli moja kumfukuza uanachama .Mbunge Seif kwa mujibu wa Ibara 83(4) na 83(5) za Katiba ya CUF-Chama Cha Wananchi  ya mwaka 1992 Toleo la 2019",amesema.

"Ikiwa Leo ni siku ya kusherehekea miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Bila Mapinduzi ya Zanzibar tusingekuwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mapinduzi ya Zanzibar ndiyo yaliyozaa Muungano wetu.Uhusianao wa karibu wa Tanganyika na Zanzibar ni wa kihistoria.Muungano wetu ni msingi muhimu wa amani na utulivu wa nchi yetu,tukamilishe upatikanaji wa Katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi ambayo itasaidia kutatua kero za Muungano", amesema Prof.Lipumba

Hata hivyo amewataka Watanzania kufahamu vizuri kuwa historia na jiografia ya nchi yetu ndiyo inatuunganisha."Tuuenzi Muungano wetu Tusibaguane,Wanasiasa  tuwe makini na tusitumie upande wa Muungano unaotoka kama kete ya kujijengea umaarufu kisiasa na kubomoa Muungano.



Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE