DEREVA WA LORI ALIYESAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO



Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline 
IRINGA

MAHAKAMA  ya Hakimu mkazi mkoa wa Iringa imemuhukumu kwenda jela miaka  mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 20 dereva wa gari aina ya lori  scania namba T 631 CNF Boniface Mwanjokolwa kwa kosa la kusafirisha wahamiaji  haramu 62 raia wa Ethiopia kinyume na sheria.

Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya mkoa wa Iringa  Honorios Kando alisema kuwa mshtakiwa amekutwa na hatia ya kusafirisha wahamiaji haramu kinyume na sheria no. 46 kifungu kidogo  cha 1 C cha uhamiaji no 54 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016.

Akirejea kusoma kesi namba 24260 ya mwaka 2024 iliyokuwa inamkabili mfungwa Boniface Mwanjokola hakimu Kando alisema kuwa mfungwa  alitenda kosa hilo august 2I mwaka 2024  katika eneo la sabasaba Mafinga barabara kuu ya Iringa-Mbeya akiwa anasafirisha wahamiaji haramu 62 raia wa Ethiopia wakielekea Kyela mkoani Mbeya kwa kutumia gari aina ya Lori scania aliyokuwa akiliendesha.

Hakimu amesema mahakama ilimtia hatiani mshitakiwa huyo ambaye kwa sasa ni mfungwa na kabla ya kusomwa hukumu alipewa nafasi ya kujitetea ndipo alipoiomba mahakama kumpa adhabu nafuu kwa kuwa kosa lake hilo ni kwanza na anafamilia inayomtegemea.
Hakimu alisema alipoulizwa muendesha mashtaka kuhusu taarifa za mshtakiwa ambaye ni mfungwa alisema hakuwa na taarifa zozote za kiuhalifu zaidi ya kosa hilo hivyo muendesha mashtaka aliiomba mahakama kutoa adhabu kali Ili iwe fundisho kwake na kwa wengine.

Hakimu Kando amesema kuwa mahakama  imezingatia taarifa hiyo ya mshtakiwa na muendesha mashtaka hivyo mahakama imemuhukumu kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 20 ambayo anaruhusiwa kulipa kidogokidogo na ataendelea kusalia magereza hadi atakapo maliza kuli fine hiyo huku lori lililokutwa likisafirisha wahamiaji hao likitaifishwa..
Aidha hakimu Kando alimwambia mfungwa huyo kuwa rufaa ipo wazi kama atakuwa hajaridhishwa na maamuzi ya mahakama.

 Baada ya hukumu kusomwa na kuamuru askari amchukue ndipo mfungwa huyo alipoomba kupunguza deni la faini aliyotajiwa, mahakama ilimruhusu afuatane na askari ambaye atampa utaratibu.


Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE