MAKADIRIO YA MATUMIZI YA SERIKALI 2025/2026 NI SH. 56.49 TRILIONI

Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline

‎Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amesema makadirio ya matumizi ya Serikali ya kwa mwaka 2025/2026 ni Sh56.49 trilioni.

‎Akiwasilisha bajeti hiyo bungeni leo Juni 12, 2025 Dk Chemba alisema bajeti hiyo inajumuisha stahiki za watumishi na michango ya pensheni (Serikali Kuu) Sh9.17 trilioni na ununuzi wa bidhaa na huduma sh5.58 trilioni.

‎“Malipo ya riba za mikopo Sh6.46 trilioni na ruzuku (subsidies & transfers) kwa taasisi za Serikali, mashirika ya umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa Sh22.17 trilioni,” amesema Dk Mwigulu.
‎Aidha, Dk Mwigulu ambaye aliwasilisha bajeti hiyoya kurasa 253 kwa takribani saa mbili na nusu, amesema Serikali inatarajia kutumia Sh7.72  trilioni kugharamia malipo ya mtaji kwa deni la ndani na nje.




Comments

Popular posts from this blog

MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, SPIKA ATOA MATUMAINI MAPYA USAWA WA KIJINSIA

‎Wingu Africa appoints Prasad Acharya as Director of Sales for Tanzania ‎

ACCELERATED ENTRY : HOW EAST AFRICA LEAPFROGGED INTO THE CLOUD AGE