DEREVA WA LORI ALIYESAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline IRINGA MAHAKAMA ya Hakimu mkazi mkoa wa Iringa imemuhukumu kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 20 dereva wa gari aina ya lori scania namba T 631 CNF Boniface Mwanjokolwa kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu 62 raia wa Ethiopia kinyume na sheria. Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya mkoa wa Iringa Honorios Kando alisema kuwa mshtakiwa amekutwa na hatia ya kusafirisha wahamiaji haramu kinyume na sheria no. 46 kifungu kidogo cha 1 C cha uhamiaji no 54 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016. Akirejea kusoma kesi namba 24260 ya mwaka 2024 iliyokuwa inamkabili mfungwa Boniface Mwanjokola hakimu Kando alisema kuwa mfungwa alitenda kosa hilo august 2I mwaka 2024 katika eneo la sabasaba Mafinga barabara kuu ya Iringa-Mbeya akiwa anasafirisha wahamiaji haramu 62 raia wa Ethiopia wakielekea Kyela mkoani Mbeya kwa kutumia gari aina ya Lori scania aliyokuwa akiliendesh...