Posts

Showing posts from October, 2023

TBA KUSHIRIKISHA SEKTA BINAFSI KWENYE MIRADI

Image
Na Mwandishi wetu,MwelekeoMedia. Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imepanga kushirikisha sekta binafsi katika miradi yao ili kusaidia kuondoa changamoto ya nyumba kwa watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla Akizungumza leo jijini Dar es Salaam octoba 16,  baada ya kutembelea miradi mitatu ya TBA,  Mkurugenzi wa Idara ya Miliki  TBA, Said Mndeme amesema kuwa mahitaji ya nyumba yamekuwa yakiongezeka kila mwaka. "Machi mwaka jana Rais Dk.Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa nyumba za Magomeni Kota, alitutaka TBA na taasisi nyingine za Serikali zinazioshughulikia ujenzi wa makazi ya watu kushirikiana na sekta binafsi za nje au ndani kwani  Kwa kufanya hivyo zitaweza kuendeleza makazi bora kwa haraka kuliko kusubiri Serikali kukusanya fedha ambazo haziwezi kukidhi uhitaji wa haraka wa makazi hayo, " amesema. Amesema agizo hilo la Rais Dk. Samia liliungwa mkono na wabunge  ambao  waliishauri TBA, kushirikiana na sekta binafsi ili kuongeza uwezo wa kujenga ny...

NIC YAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE NDANI YA MIAKA 60,YAAHIDI KUBORESHA HUDUMA KWA WATANZANIA

Image
 Na Mwandishi wetu,MwelekeoMedia. SHIRIKA  la Bima la taifa NIC katika kutimiza miaka 60 tangu kuazishwa kwake  imesema itahakikisha inaendelea kuboresha huduma zake kwa kubuni huduma mpya Kwa  kushirikiana zaidi na jamii ili kuhakikisha elimu ya Bima inamfikia kila mmoja. Hayo yamesemwa leo octoba 16 jijini Dar es Salaam na  mtendaji mkuu wa NIC Elirehema Doliye wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao kilichowakutanisha  viongozi na watendaji wa wakuu wa timu ya  yanga na wachezaji. Pia amesema maadhimisho ya miaka 60 ya shirika hilo yamekua ya manufaa makubwa kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali katika kuliinua na kuliendeleza shirika ili kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na Bima. "Leo tunaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa shirika hili ambapo tunajivunia mafanikio makubwa ambayo tumeyapa kwa kipindi chote lakini pia tumekuja na mikakati itakayosaidia katika kuandaa miaka mingine 60 ijayo"amesema Doliye. Amesema moja ya vi...

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NCHINI AMEITAKA KAMPUNI YA SUMAJKT BOTTLING LTD KUONGEZA UBINIFU NA UBORA WA BIDHAA .

Image
 Kampuni ya SUMAJKT Bottling co. Ltd, inayozalisha maji ya Uhuru Peak Pure Drinking Water, imezindua mikondo miwili ya uzalishaji maji na Muonekano mpya wa chupa za maji ya Uhuru Peak,  Akizungumza jijini Dar es Salaam Leo Octoba 16 Mkuu wa wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali CDF Jacob John Mkunda amesema  Serikali ina matarajio makubwa na Jeshi la kujenga Taifa JKT na Jeshi la wananchi. Amesema  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatambua na kutembea kifua mbele kutokana na mchango mkubwa unaotokana na shughuli zinazofanywa na  Jeshi hilo hasa katika swala zima la malezi kwa vijana. Jenerali Mkunda amefafanua kuwa  kutokana na Serikali kutambua Mchango wa Jeshi hilo imeweza kulipatia Jeshi hilo la  Suma Jkt mradi wa ujenzi wa nyumba 5000 Jijini  Dodoma na Mradi wa kulinda bomba la Mafuta hoima. Jenerali Mkunda ametoa wito kwa Suma Jkt kuendelea kubuni mikakati zaidi na kuboresha bidhaa ili  ziweze kukidhi soko la ndan...

EMIRATES SKYCARGO YAENDELEZA UZOEFU WAKE WA KIBUNIFU KWA WATEJA KWA KUTUMIA CARGOAI

Image
Na Mwandishi wetu,MwelekeoMedia Shirika la ndege la EMIRATES kupitia Emirates SkyCargo sasa imekuja na suluhisho kwa wateja wake kupitia soko la CargoAi na CargoMART, ikisonga mbele zaidi katika uzoefu wa digital kwa wateja kwa kurahisisha mchakato wa kuagiza mizigo huku mteja akiwa na taarifa halisi za mzigo wake kila hatua.  Ushirikiano huu ulianzishwa Uholanzi, Hispania, na Ufaransa, na utawafikia wateja katika nchi zilizochaguliwa barani Ulaya, Amerika, Afrika, Mashariki ya Mbali, na Australasia katika miezi ijayo.Kupitia suluhisho la CargoMART, wateja watapata ratiba za Emirates SkyCargo, viwango vya ushuru na mikataba, pamoja na upatikanaji wa wakati halisi wa mzigo hadi uliopo, kuruhusu uagizaji mara moja saa 24/7. Ushirikiano huu unasaidia ufanisi na usahihi zaidi. Mara tu mfumo utakapokuwa na uendeshaji kamili, zaidi ya wakala wa mizigo 10,000 kwenye kanzidata ya CargoAi watapata upatikanaji. Nabil Sultan, Makamu wa Rais Mkuu wa Idara, Emirates SkyCargo, alisema: "Tunavyo...

ORBIT SECURITIES YAWAITA WACHIMBAJI KUWEKEZA KATIKA SOKO LA HISA

Image
Na Mwandishi wetu,Mwelekeomedia. Fortius Rutabingwa ambaye ni mkuu  wa kitengo cha utafiti ,masoko na Maendeleo kutoka kampuni ya Orbit Securities limited   amesema orbit security ni kampuni ya wakala wa Soko la Hisa na wamekuja Kwa mara ya kwanza kwenye maonyesho  ya kimataifa ya sita ya  teknolojia ya madini yanayofanyika mkoani Geita Kila mwaka. Amesema kuwa wao kama orbit wameshiriki kwa mara kwanza na malengo ni kuwaelimisha washiriki hasa wadau wa sekta ya madini juu ya fursa zilizopo kwenye soko la Hisa au mitaji ambapo kwenye upande wa uwekezaji kwenye hisa na upande wa hati fungani watu wanoshiriki sana kwenye biashara za madini wengi huwa wanapata pesa nyingi Kwa ghafla au Kwa mkupuo hivyo wanaonyeshwa ni fursa zipi ambazo wanaweza kuweka pesa zao na zikawa salaama. Rutabingwa ameyasema haya Septemba 30 mwaka huu kwenye kilele cha maonyesho ya sita ya teknolojia ya madini ambayo yanafanyika mkoani Geita. Rutabingwa Amefafanua kuwa kuweka pesa kwenye en...

BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO YAWAHAKIKISHIA SOKO LA UHAKIKA WAKULIMA NCHINI

Image
Na Mwandishi Wetu, MwelekeoMedia  Francisco Amos,Afisa mauzo na usambazaji kutoka Bodi ya nafaka na  mazao mchanganyiko Kanda ya ziwa amesema licha ya kuwa ni mara Yao ya kwanza kushiriki maonesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini mkoani Geita,wameridhishwa na ubora wa maonesho hayo kwani yamewakutanisha na wadau wapya ikiwa ni pamoja na kujipanua zaidi kwa wananchi. Amesema kuwa wananchi wengi walipata fursa ya kufika kwenye Banda lao na Kwa ujumla walipenda huduma na bidhaa ambazo walikuja nazo kwenye maonyesho hayo. Amos ameyasema hayo septemba 30 mwaka huu katika hitimisho la maonyesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya madini ambayo yanafanyika Kila mwaka mkoani humo . Amos Amesema licha ya kwamba ni mara yao ya kwanza kushiriki kwenye maonyesho hayo lakini yamewapa picha nzuri kwamba wakati mwingine waje vizuri zaidi  nakwamba  wananchi wamependa bidhaa na huduma na wameonyesha uhitaji mkubwa zaidi. "Kwakifupi naweza kusema maonyesho yamekuwa tofa...