MAVUNDE AIPONGEZA KAMPUNI YA BLUE COAST KWA UTENDAJI WAKE ULIOTUKUKA
Na Prosper Rutayuga,MwelekeoMedia Serikali imesema itaendelea kusimamia sheria ya Local contect ili kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali zao ikiwemo madini ya dhahabu . Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Antony Mavunde alipomtembelea mmoja wa wawekezaji wazawa mkoani Geita ,Athanas Inyasi anaemiliki kampuni ya blue coast ili kujionea namna alivyonufaika na sheria ya Local contect ambapo amewasisitiza wafanyabiashara ,wachimbaji kujitokeza kuomba zabuni . "Nitoe rai kwa makampuni mengine yakitanzania kuchangamkia fursa hii sisi kama tutahakikisha tunaisimamia sheia hii vizuri ili watanzania wengi zaidi waweze kunufaika tunahitaji kuwaona akina mzee Inyasi wengi zaidi kama alivyomsema mkuu wa Mkoa ili mwisho wa siku tuweze kuyaona matokeo ya uchumi wa madini katika maisha ya watanzania na kupitia uchumi huu tuweze kukuza pia uchumi wa tanzania na jambo hili linawezekana",amesema Mavunde. Aidha Waziri Mavunde amesema kuwa...